June 14, 2021


 NYOTA wa kikosi cha Yanga, Saido Ntibanzokiza amesema kuwa wana imani watafanya vizuri kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Biashara United.

Mchezo huo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho unatarajiwa kuchezwa kati ya Juni 28 ambapo mshindi wa mchezo huo atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Simba na Azam FC.

Raia huyo wa Burundi amesema:"Tunajua kwamba Biashara United ni timu imara na inafanya vizuri lakini hatutaweza kuwaacha waweze kushinda kirahisi kwani nasi tunahitaji ushindi.

"Kikubwa ni kuona kwamba tunaweza kufikia malengo ambayo tumejiwekea kwa kupambana kwa mechi ambazo zimebaki kikubwa mashabiki watupe sapoti," amesema.

Yanga ilitinga hatua ya nusu fainali baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons kwa bao la Yacouba Songne ambaye alitumia pasi ya Saido.

4 COMMENTS:

  1. Hapana, ilitinga nusu baada ya kuifunga Mwadui

    ReplyDelete
  2. Hahahahaha hawa waandishi bhanaaa utafikiri mtu anaandika message na kutuma,
    Inamana hakuna editors au.
    SalehJembe jarbu kuimprove basi hata kidg makosa ya mwaka juz Hadi leo yanajirudia..
    Yanga alitinga nusu fainali baada ya kuifunga Tanz prsn au Mwadui???

    ReplyDelete
  3. Huyo Saido yumo katika atiati ya kutemwa na yumo katika majaribio ya kujionesha kuwa anaionea uchungu yanga ili anusurike na abakie

    ReplyDelete
  4. Waandishi humu ni vilaza, suala likipitisha wiki mbli tu ukiwaambia waliandikie taarifa wataandika uharo tupu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic