June 5, 2021

 


BAADA ya Klabu ya Yanga kutoa taarifa 
kuwa Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (Cas) imeanza kusikiliza pingamizi la awali la shauri la kimkataba la kiungo Bernard Morrison wa Simba, mchezaji huyo amefunguka mazito.


Akizungumza kwa hisia juu ya kile ambacho kinaendelea baina yake na Yanga, Morrison alisema anachofikiri kwa sasa ni kwamba viongozi wa Yanga wanataka kumpoteza mazima kwenye ardhi ya Tanzania.


Akizungumza na Championi Ijumaa, Morrison alifafanua kuwa anachohisi kwenye moyo wake, Yanga hawataki arudi tena kwenye timu yao na hata mashabiki hawatamani tena kuona hilo likitokea, ila jambo pekee wanalotaka ni yeye kutocheza tena soka kwenye timu yoyote Tanzania.


“Nahisi viongozi wa Yanga hawataki kuona nikiendelea kuwepo Tanzania au nikicheza kwenye timu nyingine hapa. Nafikiri huo ndiyo mpango wao, kwa sababu sidhani kama wanahitaji nirudi tena kwenye timu yao.


“Maana hata mashabiki na wanachama sidhani kama wanahitaji kuona hilo likitokea. Siwezi kusema kuwa ni wivu au hawataki kuona nikiwa Simba, mawazo yangu yanaona kuwa wanataka niondoke kabisa hapa,” alisema Morrison.


Kwenye taarifa ya Yanga ilieleza kuwa Cas wangetoa majibu wa mwenendo wa kesi hiyo juzi Juni 2, jambo ambalo halikufanyika na hakuna taarifa yoyote kutoka ndani ya Yanga ambayo ilitolewa juu ya shauri hilo.

7 COMMENTS:

  1. Replies
    1. kwani wachezaji wangapi wamefanya alichokifanya morison na wala hawakuchukuliwa hatua kama zinavyochukuliwa sasa hivi kwake,,tatizo lake ameondoka na kuendelea kuleta nyodo,kejeli,vijembe,maudhi kwa club ya yanga,sasa yanga wanataka kumuonyesha kuwa hii ni timu ya namna gani,tena hii imechangiwa na msemaji wake na ndio alikuwa anampa jeuri..

      Delete
  2. yeye si alifanya udanganyifu na kuhujumu timu yetu tena akawa analeta zarau basi atajua Yanga ni nani.

    ReplyDelete
  3. Hana utu Morrison fedha ni za kupita tu ,,hivi gadiel mbaga yupo wap

    ReplyDelete
  4. Utopolo pigeni Domo huku mkiendelea kugongwa kwenye mechi nakwenye usajili pia...

    ReplyDelete
  5. Yote hayo yanakuja sababu uto haifanyi vizur wakati mnyama anafanya vizur ndani na nje.... Utopolo acheni wivu usio wakimaendeleo

    ReplyDelete
  6. Uto wana wivu mbaya Sana ndo maana hata muongola wanataka akirudi timu yoyote bongo ndani ya miaka 4 wapewe mil. 400

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic