June 30, 2021

 


UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba, Julai 3 watapata ushindi kutokana na maandalizi ambayo wameyafanya huku wakiwataka watani zao wa jadi kutobadili muda.

Ikumbukwe kwamba mchezo wa Julai 3 ulipaswa kuchezwa awali Mei 8 ila uliyeyuka mazima baada ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kueleza kwamba kuna mabadiliko ya muda.

Ule wa awali ulipangwa saa 11:00 jioni ila masaa machache kabla ya mchezo huo kuchezwa huku mashabiki wakiwa wameanza kuingia taarifa kutoka TFF kupitia kwa Ofisa Habari, Cliford Ndimbo ilieleza kuwa mchezo huo utachezwa saa 1:00 jioni, jambo ambalo Yanga waliweka wazi kwamba hawatacheza muda huo kwa kuwa ni kinyume cha kanuni.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz ameweka wazi kwamba hawana hofu na mchezo wao wa watani wa jadi ila jambo la muhimu wasibadili muda.

"Hatuna mashaka na kikosi chetu na kwenye mechi zetu ambazo zimebaki tuna amini kwamba tutafanya vizuri bila mashaka.

"Kikubwa ni kwamba wasibadili muda wafuate utaratibu ambao umewekwa na kusiwe na makandomakando," amesema.

Kwenye msimamo wa ligi, Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ipo nafasi ya pili na pointi 67 huku Simba ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 73.

5 COMMENTS:

  1. Kwa hiyo anayepanga na kubadili muda ni simba, akili za kiutopolo hizi. Pamoja na barua ya TFF kuweka wazi kuwa walipokea taarifa toka serikalini ikiwataka kusogeza muda bado mtu na akili zake tena kiongozi anaropoka upuuzi, duh! Hii sasa aibu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndio ni mikia kwani wana tawi fff, usijifanye hujui

      Delete
  2. sijui kwanini utopolo wanajisahaulisha! kama ni kweli simba wana tawi tff, basi ni kama lilelile walilokuwa nalo wao wakati wa Malinzi.

    ReplyDelete
  3. Tangazo lilisema serikali ndio ilisogeza muda sio TFF, na serikali waziri wa michezo ni yanga garagara, sasa simba anaizidi serikali?

    ReplyDelete
  4. Matopolo wanasifika kwa wingi wa matamko

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic