UONGOZI wa Yanga umewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti kubwa timu yao katika mchezo wao wa kirafiki unaotarajiwa kuchezwa Juni 6 saa 1:00 usiku.
Mchezo huo utakuwa wa kirafiki ikiwa ni lengo la Kocha Mkuu, Nassreddine Nabi kuwaimarisha wachezaji wake ambapo watamenyana na African Lyon.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa mashabiki wajitokeze kuipa sapoti timu yao.
"Mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu yao kwani tuna mchezo wa kirafiki dhidi ya African Lyon utachezwa Uwanja wa Azam Complex, " amesema.
Kiingilio katika mchezo huo mzunguko ni 3,000 na VIP ni 5,000.
Kishindo chote hicho kumbe mnacheza na African Lyon kama vile mnajipima na timu ya Azam ili washinde tu halafu wajisifu
ReplyDeleteIkiwa ndio wanajitaysrisha na mchezo wao na Simba ili kuchukuwa ubingwa basi wsjipime na timu ya kiwango kinachokaribia cha Simba na sio timu iliyodhuks daeaja. Woga sana
ReplyDeleteWanaohamasishwa sio mikia kupinda aka paka mweusi!!
ReplyDelete