UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba utapambana kupata pointi tatu kwenye mchezo wao ujao dhidi ya Ruvu Shooting unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
Wakati huu ligi imesimama kwa muda kupisha maandalizi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi unaotarajiwa kuchezwa Juni 13, Uwanja wa Mkapa.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kila kitu kinakwenda sawa na wachezaji wanapewa majukumu chini ya Kocha Mkuu, Nassredine Nabi.
“Kwa mechi ambazo zimebaki ikiwa ni pamoja na ule dhidi ya Ruvu Shooting tunahitaji pointi tatu kikubwa ni maandalizi na hilo linaendelea kwa sasa.
"Mashabiki watupe sapoti kwa ajili ya mechi zetu ambazo zimebaki na tunahitaji kushinda. Kikubwa ni kuona kwamba tunapata ushindi," .
Mchezo wao ujao utakuwa ni Juni 17, Uwanja wa Mkapa ni dhidi ya Ruvu Shooting, mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Yanga 2-1 Ruvu Shooting.
Katika msimamo Yanga ipo nafasi ya pili na ina pointi 61 inakutana na Ruvu Shooting iliyo nafasi ya 10 na pointi 37.








Ili tuupate ubingwa
ReplyDeleteBila ya ubingwa na tukamuona mnyama ndie aliyeubeba basi jezi hazitouzika
ReplyDeleteTukimfunga ruvu kisha tukapewa zile 3 za mezani, ubingwa tayar
ReplyDelete