KLABU ya Arsenal inayonolewa na Kocha Mkuu, Mikel Arteta imekamilisha usajili wa kiungo kutoka Klabu ya Anderlecht, Albert Sambi Lokonga kwa dili la muda mrefu.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21 atasafiri na timu kuelekea Florida na timu hiyo kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2021/22 siku ya Jumatano.
Katika timu yake ya Ubelgiji aliweza kutokea kwenye kikosi chake mara 78 ambapo alikuwa akicheza chini ya nahodha wa zamani wa Manchester City, Vincent Kompany na aliweza kucheza hapo kwa muda wa miaka 10.
Kiungo huyo amesema kuwa kwake ni hatua kubwa kuweza kufikia sehemu hiyo na ikiwa ni mara yake ya kwanza kuhama kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine kufanya kazi na atapambana ili kufanya vizuri.
"Ni hatua kubwa kwangu kwa sababu nimecheza ndani ya Anderlecht kwa muda wa miaka 10 inakuwa ni mara yangu ya kwanza kuwa kwenye nchi nyingine na ninajiskia kujiamini," .
0 COMMENTS:
Post a Comment