July 19, 2021


 MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Simba, John Rafael Bocco kwa msimu wa 2020/21 ni mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) baada ya kufikisha jumla ya mabao 16.

Bao lake la 16 alipachika jana Julai 18, Uwanja wa Mkapa wakati timu hiyo ikimaliza mechi ya mwisho kwa msimu mbele ya Namungo FC.

Ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 4-0 Namungo ambapo mabao mawili yalifungwa na Chris Mugalu na moja lilipachikwa na Meddie Kagere huku yeye akipachika dk ya 90+3 kwa penalti.

Nyuma yake kuna mshambuliaji mwingine wa Simba, Chriss Mugalu mwenye mabao 15, mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dude anashika nafasi ya tatu akiwa na mabao 14 wakati Medie Kagere wa Simba ana mabao 13.


Kwa mara nyingine tena tuzo ya kiatu cha mfungaji bora kinakwenda Simba baada ya msimu uliopita Kgere kutupia mabao 22 na msimu huu anayo 13 yupo zake ndani ya Simba.


Pia timu hiyo imefanikiwa kutetea taji lake la ligi ambalo ilitwaa msimu wa 2019/20 ikiwa ni mara ya nne mfululizo.

2 COMMENTS:

  1. Mwandishi uliihariri hii taarifa kabla ya kuipost? Hebu isome tena uunganishe maudhui ya para ya pili kutoka mwisho

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic