MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kuwa katika mechi zao ambazo zimebaki watapambana kupata pointi tatu.
Ikiwa imecheza jumla ya mechi 32 imekusanya pointi 38 ipo nafasi ya 10 na kinara ni Simba mwenye pointi 73.
Ruvu Shooting imekuwa kwenye mwendo wa kusuasua katika kusaka matokeo msimu huu wa 2020/21 jambo ambalo linawafanya wasiwe na uhakika wa kubaki ndani ya ligi ikiwa watashindwa kupata matokeo kwenye mechi ambazo zimebaki.
Akizungumza na Saleh Jembe, Bwire amesema:"Tupo tayari kwa ajili ya mechi ambazo zimebaki na tuna amini kwamba tutapata matokeo chanya, mashabiki watupe sapoti kwani tunajua kwamba wanahitaji matokeo chanya.
"Kikubwa ni kuona kwamba kwenye kila mchezo wetu ambao tutacheza wanajitokeza kwa wingi na kutupa sapoti hatuna tatizo kabisa kwetu na wachezaji wapo vizuri,".
Mchezo wao ujao ndani ya ligi ni dhidi ya Namungo FC ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mabatini.
0 COMMENTS:
Post a Comment