KOCHA mkuu wa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Kim
Poulsen amefunguka kuwa ana matumaini makubwa michuano ya kombe la Mataifa ya
Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) chini ya miaka 23, yatawaongezea ufanisia
zaidi wachezaji wake kuelekea kwenye maandalizi ya michezo ya kusaka tiketi ya
kombe la dunia.
Ijumaa ya Julai 16, mwaka huu Poulsen alitangaza kikosi cha
wachezaji 20 wanaotarajiwa kuiwakilisha Tanzania katika michuano hiyo mikubwa
kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.
Michuano hiyo kwa mwaka huu tayari imeanza rasmi kutimua
vumbi juzi Jumapili ambapo inafanyika nchini Ethiopia.
Akizungumzia mipango yao, kocha Poulsen amesema:
“Tuna matumaini makubwa na vijana ambao tumewajumuisha katika kikosi chetu cha
U23, hii ni kwa sababu kikosi hiki kina nyota wengi wenye vipaji na uzoefu
mkubwa wa mashindano mbalimbali.
“Binafsi naamini
tutafanya vizuri kwenye michuano hii, lakini pia tutaitumia kama sehemu ya
maandalizi kuelekea kambi yetu ya mwezi Agosti ambayo tutaitumia kwa ajili ya
maandalizi ya michezo ya kusaka tiketi ya kushiriki michuano yua kombe la
dunia.”
Na TFF hii? Mpaka kufa
ReplyDeleteUtopolo
DeleteUnataka tff itoke mbinguni au? Iliyofanikisha kucheza mashindano makubwa ni ipi? Kuweni na shukurani msiwe na akili za kiutopolo
ReplyDelete