July 6, 2021



MOHAMED Samatta, nahodha msaidizi wa KMC amesema kuwa kesho kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba wataibuka kivingine toafuati na mchezo wao uliopita.

KMC itakuwa na kibarua kesho kwenye mchezo wao wa ligi dhidi ya Simba ambao ni wa mzunguko wa pili  baada ya dk 90 kukamilika na ubao kusoma Simba 1-0 katika ule mchezo wa mzunguko wa kwanza.

Samatta ambaye ni kaka wa nahodha wa Stars, Mbwana Samatta, amesema kuwa mchezo wao dhidi ya Simba utakuwa na ushindani mkubwa ila wamekubaliana kufanya vizuri ili kupata pointi tatu muhimu.

"Mchezo wa kwanza tulipoteza na tunajua kwamba wametoka kupoteza mchezo wao uliopita hivyo nasi tutakuja kivingine, kikubwa ni kuona kwamba tunapata pointi tatu.

"Ni timu bora tunajua kwa kuwa tuliona hata ilipocheza kwenye mchezo wao uliopita lakini sisi tunajiangalia wenyewe kwanza hatufikirii kuhusu mchezo wao ambao umepita.

"Inaweza ikawa ni asilimia 20 hivi tukachukua kutoka kwao kwa namna ambavyo walicheza mchezo wao uliopita ila haina maana kwamba tutaangalia kwa namna kubwa zaidi tutajiangalia sisi wenyewe," . 

Kwenye msimamo KMC ipo nafasi ya 6 ina pointi 42 inakutana na Simba iliyo nafasi ya kwanza na pointi 73.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic