IMETHIBITISHWA kuwa uongozi wa Yanga upo kwenye mazungumzo na kiungo wa kimataifa wa Ghana anayecheza soka la kulipwa kwenye Klabu ya Cleopatra inayoshiriki Ligi Kuu ya Misri, Kwame Bonsu ili kumsajili kwa ajili ya msimu ujao wa 2021/22.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Yanga
kimelitonya Championi Ijumaa, kuwa tayari
mabosi wa klabu hiyo wamekubali kuliweka jina la kiungo huyo wa Ghana ambaye amesaliwa na
mwaka mmoja tu kwenye mkataba wake wa
Cleopatra, katika listi ya nyota wapya
wanaotarajiwa kusajiliwa kwa ajili ya msimu
ujao wa Ligi Kuu Bara.
“Ni kweli uongozi kwa kupitia kamati yetu ya
usajili umekubaliana na maamuzi ya
kujumuisha jina la kiungo wa Ghana, Kwame
Bonsu kwenye listi ya nyota wapya ambao
wanatarajiwa kusajiliwa kwa msimu ujao.
“Hii ni baada ya kumfuatilia na kugundua kuwa
ni miongoni mwa viungo bora Afrika, lakini pia
ni kiungo mwenye uzoefu mkubwa na
michuano mikubwa, akiwa tayari ameshacheza
kwenye timu kubwa kama Esperance ya Tunisia
na Asante Kotoko ya Ghana.”
Akizungumzia kuhusu usajili wa kiungo huyo,
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya
Yanga, Thabit Kandoro, alisema: “Kwa sasa
tumesitisha kwa muda kuzungumzia masuala ya
usajili, kwa kuwa bado tuna kibarua cha
mchezo wetu wa fainali ya Kombe la FA dhidi ya
Simba Julai 25, mwaka huu na tutazungumzia
masuala ya usajili baada ya mchezo huo
kukamilika.”
Nyota huyo anakuja kuiimarisha Yanga baada
ya timu hiyo kufanikiwa kusuka safu imara ya
ushambuliaji ambayo inaelezwa itaongozwa na
Wacongo, Heritier Makambo, Fiston Mayele na
Kazadi Kasengu.
Atakuja kufanya kazi na Nasreddine Nabi ambaye ni Kocha Mkuu wa timu hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment