July 23, 2021

 


SHAFFIH Dauda, mchambuzi wa masuala ya michezo na Mtangazaji amesema kuwa Yanga walipaswa kumpongeza mwamuzi wa kati Ahmed Arajiga na sio kuwa na mashaka naye.


Tayari kuelekea katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho kati ya Simba v Yanga,  waamuzi wameshatangazwa huku wa kati akiwa ni Arajiga.


Mwamuzi huyo alichezesha robo fainali ya Simba v Dodoma Jiji nusu fainali Simba v Azam FC ambapo katika mchezo huu, Uwanja wa Majimaji alikubali bao la Luis Miquissone lililofungwa kwa faulo ya harakaharaka.


Kupitia kwenye ukurasa wao wa Instagram wa Yanga, jana Julai 22, Yanga waliandika waraka wa kutokuwa na imani na mwamuzi wa kati kwa kile walichoeleza kuwa amechezesha mechi nyingi za watani.


Dauda amesema:"Kuhusu mwamuzi tayari itakuwa ilipangwa tangu awali ni kama ilivyokuwa kwenye uwanja, ulijulikana kabla ya kujua nani na nani watacheza.


"Kwa kusema kwamba mwamuzi amechezesha mechi nyingi za watani hapo sioni tatizo, labda wazungumze kuhusu kiwango. Kwa hilo la mechi Yanga walipaswa wampe pongezi mwamuzi kwa kuwa amechezesha mechi mingi za mashindano haya.


"Ukiweka kando siasa moja ya waamuzi wazuri ni pamoja na Arajiga hivyo jambo la kuhoji ni kiwango na sio kusema amechezesha mechi na watani,".


Fainali ya Simba v Yanga inatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma, Julai 25.

13 COMMENTS:

  1. Yanga wanamtaka Emanueli Mwandembwa wa Arusha aliewabeba kwenye mchezo wa ligi kuu Kati yao na Simba kwa Simba kunyimwa penalties mbili za wazi kabisa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. anza na mgandamizo walotoa yanga dkk 15 za mwanzo halafu weka red ya boko dkk ya 5 halafu ufikirie zingekuwa goli ngapi

      Delete
    2. Acha weee. Tulibebwa maana simba walituzidi. Lakini mwisho wa siku tulikusanya pointi tstu. Mimi siku zote huwaambia viongozi fanyeni usajili makimi lipeni mishahara ya wachezaji na makocha. HATUTOHITAJI MSAADA WA MAREFA WALA WACHAWI

      Delete
  2. Kutokana ns hofu iliyotanda katika Yanga ya kuchapwa sasa wanafanya jaribio la kutunisha misuli wakitaraji itazaa hofu na kumpata wamtakaye, lakini Yagujuuu wacheze au waingie mitini kama walivofanya katika ule mchezo wao na Simba na mechi kupangwa

    ReplyDelete
  3. Yanga hawana jioya, kila kitu lazima wakilalamikie

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ile moja bila ni nani walilalamika na ni kipi kinawakosanisha Barbara na Manara?

      Delete
  4. Safari hii imekula kwao, wasuse tuone sasa

    ReplyDelete
  5. Utopolo shida Sana Yani refa kuchezesha mechi nyingi za watani sasa hapo Kuna tatizo gani.... Angekuwa anachezesha vibaya ingekuwa sawa... Wameshazoea kulalamika kila wakati, wanataka wabebwe ili washinde maana bila hivyo uwezo hawana

    ReplyDelete
  6. Mbona mnawachagulia, wao wamesema yoyote sio arajiga. Mikia kazi kuota penalt za kupewa... hehe

    ReplyDelete
  7. Kwan mwamuzi yuko mmoja mbn TFF wanafel ss

    ReplyDelete
  8. Simba: endeleeni kuamini refa yupo upande wenu, ila baada ya mchezo ni droo ya 1-1 na penati zitapigwa Yanga atapata 4 Simba 3.
    Manara nafasi yake atawekwa mtu mwingine, na upo uwezekano mchakato wa Mabadiliko Simba ukashindikana na Mo atajitoa Simba ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Manji atarudi Yanga na Yanga watakuwa na wawekezaji 4 huyo wa nne ajulikani sasa ila atakuwa ni mtu mwenye nguvu zaidi kifedha kuliko Ghalib, Manji na Rostama. Didier Gomez ataachana na Simba kabla ya mwezi wa 10 mwaka huu, mzee mpili awe makini Corona haina maskhara na wazee.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic