ZAKARIA Thabit, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa maandalizi ya msimu wa 2021/22 yanakwenda vizuri kutokana na kuwa na mpango kazi maalumu ambao unafanyika.
Kwa sasa kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina kimeweka kambi nchini Zambia ikiwa ni kwa ajili ya kuwafanya wawe bora zaidi ya msimu uliopita.
Akizungumza na Saleh Jembe, Thabit ambaye wengi hupenda kumuita Zakazaki amesema kuwa wanatambua kwamba msimu ujao utakuwa na ushindani jambo ambalo linawafanya wapange kufanya vizuri.
"Tupo vizuri na kila kitu kinakwenda sawa, kikubwa ni kuona kwamba tunakuwa imara, kambi na kila kitu huku Ndola kinakwenda sawa," amesema.
Jana, Azam FC ilicheza mchezo wa pili wa kirafiki ilikuwa dhidi ya Kabwe Warriors na ilishinda kwa bao 1-0.
0 COMMENTS:
Post a Comment