UONGOZI wa Namungo FC umeweka wazi kwamba una mpango wa kuboresha kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao wa 2021/22 ndani ya Ligi Kuu Bara.
Ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Hemed Morocco timu hiyo ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya 9 na pointi zake 43.
Pia iliweza kuweka rekodi ya kutinga hatua ya makundi kwenye Kombe la Shirikisho lakini ilikwama kupata pointi kutokana na kushindwa kushinda mechi zake hizo.
Morocco amesema kuwa mpango mkubwa ni kuona kwamba kunakuwa na maboresho katika kikosi hicho ili kufanya vizuri msimu ujao.
"Msimu huu tumekwama kufanya vizuri mpaka pale ulipokwisha hivyo kwa ajili ya msimu ujao tunaamini kwamba tutajipanga kufanya vizuri,".
0 COMMENTS:
Post a Comment