August 3, 2021


NYOTA  Cristian Romero yupo karibu kusaini dili jipya la kujiunga na Klabu ya Spurs na yupo tayari kukwea pipa ili kuibukia London kwa ajili ya hatua inayofuata kukamilisha usajili wake.

Raia huyo wa Argentina kwa sasa anakipiga ndani ya Atalanta na ikiwa dili lake litakamilika  basi msimu ujao atakuwa ndani ya Ligi Kuu England.

 Spurs wameongeza dili lao la kupata saini yake na kupandisha dau kutoka pauni milioni 42.7 mpaka pauni milioni 50 kwa ajili ya kumpata beki huyo.

Hivyo Atalanta ambayo inashiriki Serie A inaonekana kwamba watakubali dili hilo kwani kwao lina faida na wana wachezaji ambao wamewaweka kwenye hesabu za kuwasajili.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic