September 30, 2021


 MSHAMBULIAJI  Fiston Mayele, amesema kuwa anahitaji kufunga sana kwenye mechi zake zote ambazo atacheza kwa kuwa kazi yake ni mpira na anajua furaha ya mashabiki ipo kwenye ushindi.

Mayele yupo kwenye kitabu cha kumbukumbu baada ya kuwa mfungaji wa bao pekee la ushindi kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, Septemba 25, Uwanja wa Mkapa ambapo alimtungua Aishi Manula kwa pasi ya Farid Mussa.


Nyota huyo amesema ana furaha kubwa kufunga bao katika dabi yake ya kwanza aliyoicheza msimu huu, huku akiahidi kuendelea kufunga katika Ligi Kuu Bara na mashindano mengine.

“Kuwafunga Simba siyo kama nimebahatisha, nimezoea kufanya hivyo kwenye dabi kwani nyumbani nikiwa na AS Vita nilishacheza dabi ambayo ni ngumu na yenye ushindani kama hii ya Simba dhidi ya Yanga.

“Kikubwa ninafurahia kufunga bao langu la kwanza la mashindano nikiwa na Yanga, ambalo limetupa Ngao ya Jamii.

“Niwaahidi mashabiki wa Yanga kwa kuwaambia kuwa furaha kubwa inakuja, ninafahamu ligi ni ngumu lakini nitapambana kuhakikisha tunachukua ubingwa,” alisema Mayele na kuongeza kuwa.

“Malengo yangu katika msimu huu ni kuhakikisha napambana ili kuwa mfungaji bora wa ligi na kuipatia timu yangu ubingwa, najua kila mchezaji ana malengo yake, lakini kwa upande wangu nitahakikisha ninapambania malengo yangu kwa bidii.

“Najua sio jambo rahisi, lakini biidi zaidi na kujituma ndio kitu pekee kitakachonifikisha pale ninapotaka, kama unavojua Ligi ya Tanzania ni ngumu sana na ina ushindani wa hali ya juu unayoifanya iwe bora kila siku zinavozidi kwenda, hivyo hata mimi nimejiandaa kwenda sawa na ubora wake.”

Msimu uliopita, Tuzo ya Mfungaji Bora ilikwenda kwa John Bocco wa Simba aliyefunga mabao 16. Ukitazama sasa hivi kikosi chao unaona kimeimarika katika kila idara jambo ambalo linampa mwalimu wakati mzuri wa kufanya chaguzi kwenye kikosi chake.


Jana, Septemba 29 alikuwa miongoni mwa wachezaji walioanza kikosi cha kwanza mbele ya Kagera Sugar wakati Yanga ikisepa na pointi tatu baada ya ushindi wa bao 1-0 ambalo lilifungwa na Feisal Salum.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic