September 30, 2021


 KOCHA wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa Yanga walistahili kushinda mechi ya Ngao ya Jamii kwa sababu walitengeneza nafasi moja na wakaitumia tofauti na wao, huku akisifu usajili wao.

Simba walipoteza kwa kuchapwa bao 1-0 na Yanga kwenye mchezo mkali uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Yanga walijipatia bao lao kupitia Fiston Mayele dakika ya 11 baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Farid Mussa.

Gomes alifunguka kuwa, kwenye mchezo wowote ambao kombe linakuwa mbele ni lazima timu moja ishinde na nyingine ipoteze na bahati mbaya haikuwa siku yao, Yanga wakashinda mchezo.

“Nawapongeza wachezaji wangu walicheza vizuri, lakini Yanga walipata nafasi na wakaitumia.

“Wamefanya usajili mzuri na wanatimu nzuri sana msimu huu, tunakwenda kujipanga na ligi kwa kuwa tunafahamu kuwa itakuwa ngumu,” alisema kocha huyo.

Gomes ameingia kwenye orodha ya makocha ambao wamepoteza mechi mbili kati ya tatu za Simba na Yanga ambazo zimechezwa ndani ya mwaka mmoja akiwa kama kocha mkuu.

Ilikuwa ni Septemba 25, Uwanja wa Mkapa mchezo wa Ngao ya Jamii ulichezwa na mashabiki wa Yanga kusepa na furaha.

Kwa sasa tayari Ligi Kuu Bara imeanza ikiwa ni mwendo wa mzunguko wa pili baada ya ule wa kwanza kukamilika na Simba wakiwa ni mabingwa watetezi.

4 COMMENTS:

  1. Kocha mweledi sio makocha wetu wakipoteza mechi visingizio tele.Yanga walifunga bao lao la kichawi wakapaki basi mchezo mzima.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Akili yako imejikita hapo tu ya kuamini mafanikio yoyote basi pana uchawi nyuma yake,nadhani huwa unapata shida sana mtaani na ofisini kwako pindi unapomuona mwenzako amefanikiwa akili yako huamini kuwa ni uchawi tu na sio juhudi au maarifa ndo vimembeba

      Delete
    2. Tafuta pesa mbwa wewe uachane na fikra zako za kuamini mambo ya kichawi. Kenge wewe

      Delete
  2. Kocha anatakiwa awaamini wachezaji wake aliopendekeza wasajiriiwe na wamesajiriwa Kama kibu Denis,peter Banda muhiru,sakho na wengine awape nafasi ili wawaibishe wakina mkude ,mugalu ,kagere na kapombe ambao wanabweteka hawachezi team work

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic