September 26, 2021

 


ARSENAL imesepa na pointi tatu mazima mbele ya Klabu ya Tottenham katika mchezo wa Ligi Kuu England. 


Baada ya dakika 90, Uwanja wa Emirates,  ngoma ilisoma Arsenal 3-1 Tottenham ambao walipoteza pointi tatu muhimu.


Ni mabao ya Emile Smith Rowe dakika ya 12, Pierre Aubameyang dakika ya 27 na Bukayo Saka dakika ya 34 na mabao yote yalipachikwa kipindi cha kwanza.


Ni Son Heung-min alipachika bao la kufuta machozi dakika ya 79. Kwenye mchezo huo ni Tottenham walipiga jumla ya mashuti 10 na ni manne yalilenga lango huku Arsenal ikiwa imepiga jumla ya mashuti 12 na 7 yalilenga lango.


Arsenal imefikisha pointi 9 ipo nafasi ya 10 sawa na Tottenham iliyo nafasi ya 11 kinara ni Liverpool ana pointi 14.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic