September 27, 2021


 UKIWEKA kando kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes kuonja joto ya jiwe kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii, wachezaji walifunika kwenye asilimia kubwa za takwimu.

Watani hao wa jadi wameweka rekodi yao kwa kucheza bila kuwa na ile nyomi ya mashabiki iliyozoewa huku wachezaji wote wakionekana kupaniana katika kusaka ushindi na mwisho wa siku Yanga akasepa na taji jumlajumla.

Ndani ya dakika 90, wachezaji wa Simba waliweza kupelekeshana mpelampela na vijana wa Nasreddine Nabi wa Yanga katika takwimu huku wakishindwa kutumia vizuri nafasi ambazo walizipata katika mchezo huo.  

Kwa upande wa safu ya ushambuliaji, jumla Simba ya Chris Mugalu ilipiga mashuti 15 na ni mashuti matatu yalilenga lango huku 12 yalikwama kulenga lango kwenye mchezo huo wa Ngao ya Jamii.

Kwa upande wa Yanga yenye Fiston Mayele ilipiga jumla ya mashuti 11 ni matano yalilenga lango na sita yalikwama kulenga lango na katika hayo matano ni moja lile la Fiston Mayele lililenga lango na kumshinda mlinda mlango Aishi Manula.

Kona Yanga ilipiga Saba hapa iliwapoteza mazima Simba kwa kuwa wao walipiga kona tatu pekee na zote zilipigwa na kiungo wao fundi Rarry Bwalya, katika kona hizo mbili zilikuwa na hatari zilipokutana na beki Joash Onyango ambapo ile ya kwanza iligonga nguzo na ile ya pili ilikwenda nje ya lango.

Simba ilicheza jumla ya faulo 26 na ni Taddeo Lwanga ambaye alikuwa mkata umeme alikata umeme mpaka akaonyeshwa kadi mbili za njano na kupelekea kuonyeshwa kadi nyekundu huku Yanga wakicheza faulo 18.

Kuotea hapa namba zilikuwa sawa kwa wote Yanga ilikuwa mara moja na Simba ilikuwa ni mara moja pale Uwanja wa Mkapa sawa na ilivyokuwa kwenye kadi za njano ambapo wote walionyeshwa kadi nne za njano.

 

Umiliki wa mpira, Simba iliwapoteza Yanga jumlajumla kwa kuwa walikuwa na umiliki 53 huku wapinzani wao Yanga wakiwa na umiliki asilimia 47, licha ya Simba kuwa na umiliki mzuri wa mchezo ngoma iliisha Simba 0-1 Yanga na Ngao ya Jamii ni mali ya Yanga.

1 COMMENTS:

  1. Wale wazee wa vicoments wako wapi? Ah Yanga nyinyi mbn mnaa hatari na nusu vip manara kacheza?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic