September 2, 2021


 BONDIA mzawa kutoka Morogoro, mji kasoro bahari, Twaha Kiduku hivi karibuni alishinda pambano na kujipatia gari kwa kumtwanga Dulla Mbabe amesema kuwa bondia Hassan Mwakinyo anajibiwa ulingoni.

Watu wengi wamekuwa wakiulizia pambano la Mwakinyo v Kiduku jambo ambalo Mwakinyo aliweka wazi kwamba hafikirii kufanya hivyo kwa wakati huu.

 

Kiduku amesema:-“Unajua ninachoamini mimi ni nyodo tu, ushaona, kikubwa sitaki kufocus nayo kwa sababu zile clip nimeziona anataka ajibiwe ila mimi naendelea na mazoezi kwa sababu bondia wa kweli unapomtaka lazima akubali mpigane.

 

“Muwe kama wanaume, mnapigana maisha mengine yanaendelea mbele lakini kila siku inakuwa hivyo maana ugomvi wadada na wanaume ni tofauti, wadada mmoja anaweza akamshika mwenzie mara eehee sijui hivi na hivi…dela sijui la kuazima… eeh sijui hivi na hivi.

 

“Mnajibishana mwisho siku hata kushikana hamshikani ila wanaume mmoja anaweza akapewa tusi halafu mwingine akamvaa, sasa mambo hayo yakienda mimi na huo upande wa pili yatakuwa kama ya wadada…jamani hivi mara vile sasa mimi sipo hivyo, siwezi kuongea kama mtoto wa kiume ambayo anayaweza, anajua kazi yangu ni hivi basi mnapigana, mnaendelea.

 

“Lakini kuwa na magari, magari ndiyo ya kwake kama ana maghorofa ya kwake, watu hatutaki hayo sisi tunachotaka watu waone show hivyo tu, watu wanachotaka kuona ni ladha,” Bondia Twaha Kiduku.

5 COMMENTS:

  1. Wagosi huwa hatuongeagi sana,Sie huwa tuna piga tu

    ReplyDelete
  2. Amwache mwakinyo sasa anafocus na pambano kubwa la uzito wa dunia sio hili la kugombania magari kama hao madada anao wasema🤣🤣🤣

    ReplyDelete
  3. Mwakinyo ana ndoto zake kama wew ndoto zako kupigana na Hassan bas msubir atimize ndoto zake haraf ndo umtafute

    ReplyDelete
  4. Pambano linalofuata twaa kiduku na selemani kidunda, twaa amegoma kusain wote supermiddle weight alafu unaongea kuhusu twaa anakataa kusaini🙆😂😂😂😂

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic