September 10, 2021

 


BEKI wa kati Ibrahim Ame ambaye msimu wa 2020/21 alikuwa ni mali ya Simba, msimu wa 2021/22 atavaa uzi mkali wa Mtibwa Sugar. 


Nyota huyo aliibuka ndani ya Simba akitokea Coastal Union zama zile ilipokuwa ikinolewa na Juma Mgunda ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi.


Dili lake ni la mkopo wa mwaka mmoja akitokea Simba hivyo atakuwa Morogoro akionyesha uwezo wake uliojificha kwenye miguu yake na akili zake za kichwa alizopewa na Mungu.


Anaungana na mshikaji wake Ndemla ambaye walikuwa naye Simba msimu uliopita walipofanikiwa kutwaa mataji matatu ikiwa ni lile la Ligi Kuu Bara,  Kombe la Shirikisho na Ngao ya Jamii.


Pia anaingia kwenye rekodi ya wachezaji ambao walikuwa katika kikosi kilichotinga hatua ya robo fainali katika Ligi ya Mabingwa Afrika.


Mtibwa Sugar wameachia tambo kuwa Ame akichanganya ufundi wake na sukaru bora mambo yatakuwa safi kabisa.

3 COMMENTS:

  1. Huyu si yule aliyebebwa juu kwa juu na tambo nyingi pale bandarini, kulikoni?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Siye huyo, ni wakina sarpong, fiston, na wengineo

      Delete
    2. Unaota wewe...lini Simba wamebeba wachezaji juu kwa juu kama jeneza mliowabebea kina Eng.Hersi,Kalinyo, Sarpong, Sogne, Fiston na wengineo malizia wewe Utopolo

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic