September 28, 2021

 


NGOMA imekamilika Uwanja wa Karume kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara kugawana pointi mojamoja na Biashara United. 


Ilikuwa ni kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa,  Uwanja wa Karume baada ya ubao kusoma Biashara United 0-0 Simba.


Pongezi kwa kipa namba moja wa Biashara United,  James Ssetupa ambaye aliokoa michomo yote ya hatari iliyopigwa na Simba kupitia kwa beki wao Israel Mwenda. 


Licha ya uwepo wa John Bocco na Meddie Kagere mbele, safu ya ushambuliaji ilionekana butu kwa kushindwa kupata bao katika mchezo huo. 


Aishi Manula alifanya jitihada kubwa kuokoa hatari za Biashara United iliyokuwa inamtumia Denis Nkane.


Penalti ya usiku Simba walikosa kupitia kwa Bocco iliishia mikononi mwa kipa wa Biashara United.

4 COMMENTS:

  1. Alafu mnachukua magolkipa mnaowajua taifa stars

    ReplyDelete
  2. Mungu mkubwa mtenda haki inapotakikana kutendwa haki kwani hii penalt angakosa Cris Mugalu nadhani watu wangefika pabaya pengine hata kukufuru. Hii inaonesha Gomez ni bonge la kocha na anajua nini anachokifanya. Kagere na Boko kwenye mechi na biashara wameonesha kwanini Gomezi chaguo lake la kwanza ni Mugalu kwenye washambuliaji.

    ReplyDelete
  3. Wakatii watu wengi wakilaumu Azam kutoka sare na coast Union na kuwazodoa Simba kutoka sare na biashara lakini watu wanaacha kuwapongeza coast na Biashara kwa viwango bora walivyo onesha. Huu ushindani tuliutarajia kabla ya ligi kuanza na ni Jambo zuri kuona tuliyoyatarajia yanatokea.Na kama si makandokando ya nje ya Uwanja kwenye mechi ya kagera na Yanga basi tutarajie mechi ya ushindani pia.kwa upande wangu si kuona sababu ya mechi ya Yanga na kagera kuchezwa jumatano ni kama kushawishi na kuhalalisha upangaji wa matokeo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic