September 28, 2021


 KIUNGO mkabaji mpya wa Yanga Mganda, Khalid Aucho amewaahidi mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia katika msimu huu hawataacha taji lolote la ubingwa.


Mganda huyo alitoa kauli hiyo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Kariakoo Dabi uliopigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar ambao Yanga waliwafunga Simba bao 1-0.


Katika mchezo huo, Aucho alicheza namba sita huku juu yake akisaidiana na Mkongomani Yannick Bangala Litombo.


Akizungumza na Championi Jumatatu, Aucho alisema kuwa, atafanya kile kilichomleta Yanga ambacho ni kuipa mataji ya ubingwa kwa kipindi chote atakachokuwa katika timu hiyo.


Aucho alisema kikubwa anataka kuona mashabiki wa timu hiyo wanapata furaha huku akifurahi kuwepo katika timu bora ya Yanga.


Aliongeza kuwa Ngao ya Jamii waliyoichukua Jumamosi ni mwanzo mzuri kwa wao kufanya vizuri katika msimu ujao ambao anaamini utakuwa wenye mafanikio.

“Ninafahamu mashabiki wa Yanga wana furaha kubwa ya kuona timu yao inabeba makombe katika msimu huu na kati ya hayo ni ubingwa wa ligi.


“Huu ni mwanzo mzuri kwetu Yanga kuendelea kuchukua makombe baada ya kuichukua Ngao ya Jamii dhidi ya wapinzani wetu Simba.


“Kikubwa tunahitaji ushirikiano kutoka kwa mashabiki ili kufanikisha lengo yetu ambayo ni kuchukua makombe hayo, siyo kazi rahisi lakini tutapambana,” alisema Aucho aliyeidhibiti safu ya kiungo ya Simba.



7 COMMENTS:

  1. Kubahatisha hiyo mbao bas kelele nyiingi... Subirini kesho muone kitakachowapata maana mlitumia nguvu zote ss hv hapo mlipo mna uchovu wa kutosha

    ReplyDelete
    Replies
    1. Licha ya kuacha akiba ya nguvu nyingine kwa ajili ya michezo ijayo lakini bado biashara imegoma huko Mara. Huenda mmesahau kuwa biashara ni asubuhi na jioni ni mahesabu. Kama mnasubiri tupoe msahau. Tulishaonja raha ya mataji mara 27. Tunajua nini maana yake, hatuna mpango wa kuliachia mwaka huu

      Delete
  2. Kama nynyi tu si mmeona kijichowakuta

    ReplyDelete
  3. Haha penati ya usiku, imeota mbawa!

    ReplyDelete
  4. Naona mambo yameanza mapema kupewa penalt za jion.
    Subirin yanga apewe leo muone kama mwaisa atakosa

    ReplyDelete
  5. Tunaamini juu ya kile unachokisema tunaipenda yako tunaomba mtutendee haki

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic