September 6, 2021


 BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Idd Pialali amepoteza pambano la ubingwa wa UBO dhidi ya Arvi Avci kwa TKO raundi ya sita katika pambano lililopigwa Cafetaga Sports jijini Istanbul nchini Uturuki.

 

Katika pambano hilo ambalo lilikuwa la uzito wa Walter, Pialali amepoteza kwa TKO ya raundi ya sita katika pambano la raundi kumi.

 

Akizungumza na Champion jumatatu kocha wa Bondia huyo Edward Lyemike alisema kuwa bondia wake alipoteza pambano hilo kwa sababu lilikuwa pambano la kushitukiza na hakupata muda wakutosha kujiandaa kuelekea pambano hilo.

 

Hata hivyo, ameomba radhi kwa Watanzania kwa kupoteza pambano na alisema mara baada ya kuwasili nchini wataanza maandalizi ya pambano lijalo la mwezi Oktoba dhidi ya Bondia Ramadhani Shauri.


 "Ombi langu kwa wapenzi na mashabiki wa masumbwi wazidi kuendelea kumuunga mkono kijana wao,” alisema Nicholaus.

3 COMMENTS:

  1. Yaani sababu nyingine zinachekesha sana,eti "lilikuwa ni pambano la kushtukiza na hakupata muda wa kutosha kujiandaa"...... kwani walikutana barabarani wakaambiana waende ulingoni wakazipige?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Haaa haaa haaa,, visingizio vngne cyo vya kusema et

      Delete
  2. Njaa zenu mmeziweka mbele...Hamjifunzi kwa Mwakinyo!?
    Kulikua na haja gani ya kupigana bila maandalizi?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic