September 30, 2021


 MLINDA mlango wa Yanga raia wa Mali, Djigui Diarra ‘Screen Protector’ amefunguka kuwa siri kubwa ya ubora wake katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Simba, ni kufuata maelekezo ya makocha wake, pamoja na muunganiko mzuri wa safu yao ya ulinzi.

Diarra ni miongoni mwa nyota ambao walikuwa kwenye kiwango kikubwa Jumamosi na kuisaidia Yanga kushinda taji la Ngao ya Jamii kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba, kwenye mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.

Katika mchezo wa Jumamosi, Diara alikuwa katika kiwango kikubwa ambapo alifanikiwa kuokoa mashuti matatu ya hatari yaliyolenga lango kati ya mashuti yote 15 ambayo yalipigwa na Simba katika mchezo huo.


Akizungumza na Championi Jumatatu, Diara alisema: “Kwanza kabisa nashukuru sana kumaliza mechi salama na kufanikiwa kushinda taji la Ngao ya Jamii tena dhidi ya Simba, ulikuwa mchezo mzuri na ambao kila mmoja alipambana kwa jasho na damu kwa ajili ya timu.

“Kuhusiana na kiwango changu naweza kusema siri kubwa ni kujituma mazoezini kufuata maelekezo ya mwalimu, na kushirikiana na wenzangu hasa wa safu ya ulinzi.”


Tayari kipa huyo amecheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Bara ilikuwa mbele ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba na timu hiyo ilifanikiwa kushinda kwa bao 1-0 na kusepa na pointi tatu mazima.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic