BAADA ya kupoteza pointi tatu kwenye mchezo wao wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara, Klabu ya KMC nguvu zake zote sasa ni kuelekea kwenye mchezo wao ujao dhidi ya Coastal Union.
Jana ikiwa Uwanja wa Karatu, ilishuhudia ubao ukisoma Polisi Tanzania 2-0 KMC jambo lililowafanya wapoteze furaha kwa kuziacha pointi tatu mazima.
Ni mabao ya Vitalis Mayanga ambaye aliwahi pia kuwa ndani ya KMC aliwatungua dakika ya 3 na 20 kipindi cha kwanza huku kipindi cha pili jitahada za washambuliaji wa KMC kuweka mzani sawa zilikwama pale Uwanja wa Karatu.
Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa wamepoteza mchezo wao wa kwanza mbele ya Polisi Tanzania hivyo nguvu zao wanazipeleka kwenye mchezo ujao.
Itakuwa ni Oktoba 2, pale Uwanja wa Mkwakwani dhidi ya Coastal Union ya Tanga ambayo imetoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Azam FC kwenye mchezo wao wa ufunguzi.
Ikumbukwe kwamba kabla ya mchezo wa KMC kukamilika kuchezwa Uwanja wa Karatu ulibadilishwa viwanja mara mbili ambapo awali ulitarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ushirika kisha ukapelekwa Uwanja wa Sheik Amri Abeid kisha ukaibukia Karatu.
0 COMMENTS:
Post a Comment