NYOTA wa Yanga, Ditram Nchimbi aarufu kama Duma kwa msimu wa 2020/21 alikuwa na hatari ya kufunga ama kutengeneza nafasi ya bao kila baada ya dakika 243.
Ni bao moja alifunga
ilikuwa Uwanja wa Mkapa akiwa nje ya 18 kwa mguu wake la kulia dakika ya 18 Aprili
20 mbele ya Gwambina FC ya Mwanza ambayo imeshuka daraja na msimu ujao
itashiriki Championship Tanzania zamani ilikuwa inaitwa Ligi Daraja la Kwanza.
Pasi za mabao alitoa
tatu ilikuwa mbele ya Biashara United akiwa nje ya 18 kwa mguu wa kulia ilikuwa
Uwanja wa Karume, Oktoba 31,2020.Pasi ya pili alitoa Uwanja wa Februari17,
Uwanja wa Mkapa akiwa nje ya 18 kwa mguu wa kulia mbele ya Kagera Sugar.
Pasi yake ya tatu kwa
msimu wa 2020/21 ilikuwa mbele ya Dodoma Jiji kwa mguu wa kushoto Mei 19 mbele
ya JKT Tanzania ambayo msimu ujao wa 2021/22 itashiriki Championship Tanzania,
Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Nchimbi alicheza jumla
ya mechi 25 na ni mechi tano aliyeyusha dakika 90 huku mechi 20 akikwama
kuyeyusha dakika zote 90.
Alizomaliza dakika 90
ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons, Simba,JKT Tanzania,Gwambina na Dodoma Jiji.
Ambazo hakuyeyusha
dakika 90 mwendo wake ulikuwa namna hii:- dakika 21 mbele ya Mbeya City,dakika
2 mbele ya Mtibwa Sugar, dakika 31 mbele ya Polisi Tanzania, dakika 82 mbele ya
Biashara United, dakika 8 mbele ya Gwambina, dakika 18 mbele ya Namungo, dakika
70 mbele ya Azam FC, dakika 5 mbele ya Ruvu Shooting, dakika 11 mbele ya Mwadui FC.
Dakika 1 mbele ya
Dodoma Jiji,dakika 16 mbele ya Mbeya City,dakika 45 mbele ya Kagera Sugar,
dakika 71 mbele ya Mtibwa Sugar, dakika 61 mbele ya Polisi Tanzania.
Dakika 14 mbele ya KMC,dakika 7 mbele ya
Biashara United, dakika 32 mbele ya Azam FC, dk 28 mbele ya Namungo, dk 82
mbele ya JKT Tanzania, dk 27 mbele ya Simba.
Jumla katika mechi 25
ambazo alicheza aliyeyusha dakika 973 akiwa amehusika katika mabao manne kati
ya 52 ambayo yalifungwa na timu hiyo katika mechi 34 kwa kuwa alifunga bao moja
na kutoa pasi moja ya bao.Ana wastani wa kuwa na hatari kila baada ya dakika
243.
Anacheza mechi zote???
ReplyDelete