September 9, 2021

 


IMEELEZWA kuwa baada ya mkongwe, Franck Ribery kujiunga na Salernitana ya Serie A,  nyota wa zamani wa Arsenal na Chelsea,  David Luiz huenda akaibuka hapo muda wowote. 


Salernitana imepanda Serie A msimu huu na tayari imeanza kusajili wachezaji wakongwe akiwemo Ribery mwenye miaka 37.


Taarifa zimeeleza kuwa klabu hiyo itamtangaza beki huyo ambaye watamsajili kama mchezaji huru.


Kabla ya dirisha la usajili Ulaya kufungwa, Luis alikuwa anatajwa kuwa huenda angejiunga na Benfica ya Ureno lakini ngoma ikawa ngumu..

Itakuwa ni mara ya kwanza kwa Luiz kucheza ndani ya Serie A na kwa sasa ana miaka 34.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic