September 11, 2021


 UONGOZI wa Klabu ya Yanga umethibitisha kuwa mechi yao ya kesho Jumapili dhidi ya Rivers United itapigwa bila ya uwepo wa mashabiki.

Ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo utachezwa Uwanja wa Mkapa. Jana Yanga walitoa taarifa kuhusu viingilio vya mchezo huo ila leo wametoa taarifa kwamba hakuna ruhusa ya uwepo wa mashabiki.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa CAF imezuia mashabiki kwa sababu Tanzania bado haijafikia viwango vya shirikisho hilo juu ya protokali za usimamizi wa ugonjwa wa Uviko-19.

Kwa mechi zote ambazo zitachezwa kwa wakati huu hazitakuwa na mashabiki ikiwa ni pamoja na ule wa leo wa Kombe la Shirikisho kati ya Azam FC dhidi ya Horseed FC ya Somalia.

Pia taarifa kutoka Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) imeeleza kuwa imewasiliana na timu zote zinazoshiriki mashindano ya kimataifa ambazo ni Simba, Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Biashara United na Azam FC ambazo zinawakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho.

5 COMMENTS:

  1. Tutumie ukweli ili tuaminike. Kwanza habari zilisema mashabiki wanaruhusiwa kuingia, sijui habari hizo zilipatikana wapi na sasa kuwa mashabiki hawatoruhusiwa

    ReplyDelete
  2. Yanga walitaka kulazimisha nashani walikuwa na usongo wa kupiga pesa na kujaza uwanja kuliko watani zao! In Manara's mind!

    ReplyDelete
  3. Na tunataka iwe hivyo siyo ifike Simba wanacheza mtwambie CAF imeruhusu idadi fulani Salehe Ally tunza hii siyo septemba mtwambie tofauti.Sisi yetu macho.Hii inaitwa Safari ndefu na yenye mabonde.

    ReplyDelete
  4. Ila poleni mikia AKA Makorokoro Fc ,Ni Mungu kamtwaa jina lake lihimidiwe.Ila mmempoteza mmoja wa wahuni wa Mpira.

    ReplyDelete
  5. Jembe limeondoka ila hakuna atakaeishi milele is about time.uwe mgonjwa,uwe mzima,uwe mpole uwe mtata,vyovyote vile ilivyo kifo hakichagui.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic