September 9, 2021


 DUNIA haikuweza kushtuka wala kumtambua kwa kuwa alikuwa bado mdogo hiyo ilikuwa ni Desemba 14, 1979 alipoletwa duniani huyu ni Michael Owen ambaye miguu yake ilikuwa na ushkaji mkubwa na nyavu.

Raia huyo wa England amecheza Liverpool, Real Madrid, Manchester United, Newcastle United pamoja na Stoke City bila kusahau timu yake ya taifa ya England.

Ndani ya Liverpool hapo rekodi zinaonyesha kuwa amecheza mechi nyingi ambazo ni 216 na alitupia mabao 118 kwa kuwa yeye ni mshambuliaji hata timu ya vijana ambayo amecheza ni ile ya Liverpool.

Aliposepa ndani ya Ligi Kuu England na kuibukia La Liga ilikuwa ndani ya Real Madrid ambapo huko alicheza jumla ya mechi 36 na mabao aliyofunga ni 13 kisha akarudi kwenye ligi ya England msimu wa 2005/2009 akiwa ndani ya Newcastle United.

Akiwa Newcastle United ni mechi 71 alicheza na alifunga mabao 26 alitua Manchester United 2009/2012 alicheza mechi 31 alitupia mabao matano kisha maisha yake ya soka la ushindani yalikomea ndani ya Stoke City ambapo alipachika bao moja katika mechi 8.

Jumla alicheza mechi 362 na kufunga mabao 163 na katika timu ya taifa ya England jumla alicheza mechi 89 na alitupia mabao 40.

Owen kwa sasa ni mchambuzi wa masuala ya mpira katika television na alikuwa anatumia miguu yote miwili nyota huyo mwenye miaka 41.

Kabatini ana tuzo ya Ballon d'Or aliyotwaa mwaka 2001,mfungaji bora mara mbili ndani ya Ligi Kuu England ilikuwa msimu wa 97/98 alitupia mabao 18 sawa na msimu wa 98/99.

Mataji ambayo aliwahi kuyanyanyua ni FA Cup 2001 pia alitwaa taji la English Cup mara mbili mwaka 2001 na 2003 na UEFA msimu wa 2000/01 yote akiwa na Liverpool.

Ubingwa wa Ligi Kuu England 2011, taji la English League Cup 2010 na taji la English Super Cup 2011 hya yote aliyatwaa akiwa na Manchester United.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic