September 30, 2021

 


NYOTA wa Dodoma Jiji, Cleophance Mkandala ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba ambao utakuwa ni wa mzunguko wa pili.


Dodoma Jiji imetoka kushinda bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.


Mtupiaji wa bao hilo alikuwa ni Mkandala mwenyewe aliyepachika bao lake la kwanza kwa msimu wa 2021/22 na kuipa pointi tatu muhimu.


Mkandala amesema:"Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Simba na kikubwa ni kuona kwamba tunapata pointi tatu," .


Simba ipo Dodoma imetoka kugawana pointi mojamoja  na Biashara United katika mchezo wa mzunguko wa kwanza.

1 COMMENTS:

  1. Kama vijana mliowasajili hamuwaamin basi wauzeni,timu inataka kupata muunganiko kwa ajili ya ligi kubwa ya caf champion na mechi hizi ndizo zitakazo wafanya waelewane na kujuana haswa leo nyinyi mnafanya mambo kama vile ubongo upo domant yani hamfikirii na wala hamuoni kama mnakosea,acheni mambo ya ajabu jamani simba timu kubwa vijana mliowaleta wapo sawa tunaomba wapeni nafasi na muda ndio huu.hata leo ukijaza kikosi chako ulichokikariri tunapigwa tena au suluhu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic