September 10, 2021


 MSHAMBULIAJI wa zamani wa Juventus, Mario Mandzukic ametangaza kutundika daluga akiwa na umri wa miaka 35.

Nyota huyo msimu uliopita alikuwa ndani ya Klabu ya AC Milan alikwama kufanya vizuri kutokana na kusumbuliwa na majeraha aliyokuwa nayo mpaka anatangaza kustaafu soka akiwa kikosini hapo.

Ikumbukwe kuwa aliwahi kutumikia timu ya taifa ya Croatia na alicheza jumla ya mechi 88 mpaka anastaafu mwaka 2018.

Pia mshambuliaji huyo amepita katika timu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Atletico Madrid,Bayern Munich,Milan,Dinamo Zagreb,Wolsburg,Al-Duhail,NK Zagreb na Marsonia.

Mafanikio makubwa aliyapata akiwa ndani ya Bayern Munich ambapo alitwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2012/13. Mpaka anastaafu soka aliweza kutwaa mataji 23 alitupia mabao 261 katika mechi 261.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic