September 27, 2021


 IMEELEZWA kuwa nyota wa Manchester United, Cristiano Ronaldo anampango wa kuja kuwa kocha katika timu hiyo pindi Mungu akimpa neema ya kufikisha umri wa miaka 40.

Kwa sasa nyota huyo ana umri wa miaka 36 na bado anakiwasha ndani ya uwanja na anatajwa kuendelea kuwa kwenye ubora huo mpaka atakapofikisha miaka 40.

Taarifa zimeeleza kuwa staa huyo kwa sasa ameanza kusoma ili awe kocha wa Manchester United miaka minne ijayo ila anafanya hivyo pia ili aweze kumsaidia mwanaye Cristiano Jr mwenye miaka 11 ambaye naye yupo kwenye kikosi cha vijana cha Manchester united.

Dili lake ni la miaka miwili ndani ya Manchester United ambapo alisaini akitokea Klabu ya Juventus awali alikuwa anatajwa kuibukia kwa mashasimu wa United Manchester City ila dili hilo lilibuma na sasa yupo ndani ya timu hiyo inayopambana kutwaa taji la Ligi Kuu England.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic