OFISA Mtendaji Mkuu wa Yanga (CEO), Senzo Mazingisa, amesema wamejiandaa kufanya kazi bora na kuijenga Yanga mpya na imara kwa ajili ya kuongeza chachu ya mafanikio zaidi ili kutimiza malengo yao, ikiwemo kutwaa mataji mbalimbali.
Senzo hivi karibuni aliteuliwa na uongozi wa timu hiyo kuwa CEO katika klabu hiyo kwa muda akitoka katika cheo cha mshauri mkuu wa masuala ya mabadiliko ya klabu hiyo.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Senzo alisema kuwa wao kama viongozi wamejipanga kufanya kazi kubwa ndani ya Yanga kwa ushirikiano ili kufikia malengo ya timu.
“Sisi kama viongozi tumejiwekea malengo yetu
ambayo mojawapo ni kuifanya Yanga ifikie
katika hatua kubwa ya mafanikio kwa kufanya
kazi kwa ushirikiano ili tufikie hayo malengo.
“Tumejipanga vema kabisa kuhakikisha
tunaifanya kazi hii kwa uzuri kabisa na niseme
tu kuwa sasa tunaenda kufanya kazi ya
kuifikisha katika kilele cha mafanikio ikiwa ni
pamoja na kubeba mataji ya michuano
mbalimbali,” alisema kiongozi huyo.
Leo Yanga ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa ikiwa ni hatua ya awali dhidi ya Rivers United mchezo unaotarajiwa kuchezwa bila ya mashabiki, Uwanja wa Mkapa.
Tujipange kisawasawa sio maneno tu
ReplyDeleteImeshajengeka
ReplyDelete