UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa sababu kubwa za Kocha Mkuu Didier Gomes kuhitaji mechi za kirafiki ni kupata utimamu wa mwili pamoja na kujua maendeleo ya wachezaji wake.
Kwa sasa kikosi hicho kimeweka kambi Arusha kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2021/22 na kinatarajiwa kurudi wiki hii kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya mwisho.
Pia leo Septemba 13 ni mwanzo ya Wiki ya Simba kuelekea kwenye tamasha la Simba Day ambalo linatarajiwa kufanyika Septemba 19, Uwanja wa Mkapa.
Kwenye siku hiyo ya tamasha la Simba ni mchezo wa kirafiki kati ya Simba v TP Mazembe unatarajiwa kufanyika huku utambulisho wa wachezaji pamoja na uzi mpya wa msimu wa 2021/22 utafanyika.
Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu amesema kuwa hesabu kubwa za kocha kwenye mechi za kirafiki ni kujenga utimamu wa mwili pamoja na kuona uwezo wa wachezaji wao ambao wapo kambini.
Jana Simba ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Fountain Gate na timu hiyo iliweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Mechi zote ambazo wanacheza za kirafiki ni za ndani na hawaruhusu mashabiki.
Simba kubwa nyie, oohooo!! Halafu ina mambo ya kiulaya ulaya kama barcelona yaani
ReplyDelete