UONGOZI wa Simba, umeweka wazi kuwa hesabu zao kubwa kwa msimu wa 2021/22 ni kusepa na ubingwa wa Ligi Kuu Bara mapema kwa kuwa wana kikosi imara na benchi la ufundi makini.
Kwa sasa kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes, kipo Arusha kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya msimu wa 2021/22.Akizungumza na Spoti Xtra, Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu, alisema:
“Tuna kikosi chenye wachezaji wazuri ambao wapo kwenye maandalizi kwa ajili ya msimu mpya. Jambo kubwa ni kuona kwamba yale mataji ambayo tulitwaa msimu uliopita ikiwa ni pamoja na Ligi Kuu Bara tunalichukua.
“Kwa sasa tunachokifanya ni maandalizi kwani hakuna kinachowezekana kutokea kama hakutakuwa na mipango. Benchi la ufundi tulilonalo ni la kazi mpaka vifaa pia tunavyo, hivyo mashabiki waendelee kuwa bega kwa bega na sisi.”
Nila ya shaka yupo bega kwa bega kuliko wakati wowote. uliopita na Mungu tunamuomba awe pamoja nasi tutimize malengo yetu yote
ReplyDeleteSimba Nguvu Moja.
ReplyDeleteBig up SIMBA!
ReplyDelete