September 20, 2021


UONGOZI wa Simba umewashukuru mashabiki pamoja na wadau ambao walijitokeza jana Septemba 19 kwenye siku ya tamasha ya Simba Day.

Tamasha hilo ambalo lilikuwa limefana lilihusisha watu wa aina mbalimbali ambapo mashabiki wengi wa mpira walikuwa wanalifuatilia na wale waliokuwa nje ya nchi walikuwa wanalitazama kupitia Azam Tv.

Barbra Gonzalez, Mtendaji Mkuu wa Simba amesema kuwa jambo la furaha kuona namna Wanasimba pamoja na watu wengi walivyojitokeza kwa ajili ya tamasha la Simba Day.

Kifupi tu Barbara amesema:"Asanteni Wanasimba,".

Pia kulikuwa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa ambapo ulipigwa mpira wa kazi kati ya Simba na TP Mazembe baada ya dakika 90, ubao ulisoma Simba 0-1 TP Mazembe.

Ni uzembe wa safu ya ulinzi wa Simba iliyokuwa inaongozwa na Pascal Wawa kufanya makosa ya kushindwa kulinda lango lao jambo ambalo lilisababisha maumivu dakika za jioni.

Erasto Nyoni hakuwa na chaguo alimuacha Baleke Jean dakika ya 84 akifunga bao kwa mtindo wa kubinuka na kuzama mazima nyavuni katika mchezo huo uliohudhiriwa na mashabiki wengi.

5 COMMENTS:

  1. Mpira ni mchezo wa makosa na ndio njia ya kupata mshindi na mshindwa lakini juu hayo sisi mashabiki tumefurahishwa sana na kiwango cha timu yetu katika mechi huo friendly, sio ya ubingwa bali ni ya kujipima wapi panahitaji marakibisho na kuujuwa uwezo wa wachezaji hasa wale wapya na kwa hilo tumefanikiwa 100% na hongera kikosi cha ufundi na uma uliojitokeza ambao umemtisha yule alietarajia kutetereka baada ya kuondoka kwake

    ReplyDelete
  2. Muda mrefu kambini, kujipima na timu za kutosha na kushangiliwa kote kule, bado mfungwe na timh B tena kwa Mkapa.. dhuu!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Eti timu B,una weweseka,angalia usije ukapigwa jibao la uso,mzembe wewe ngoja tarehe 25 ndio utaelewa kilichofanyika simba.

      Delete
  3. Nilipenda sana Ile TIKI TAKA hahahah

    ReplyDelete
  4. Haukuwa ni uzembe isipokuwa ili ujuwe huo uzembe au kosa lako nilazima uwazibiwe ndio kilichotokea au? Mara nyingine wata.....ila niwapongeze kwa kuujaza uwanja wa mkapa haijawai tokea,pamoja na hayo wamecheza vizuri ikizingatia timu walicheza nayo nikibwa mno kwao, Mkandawile

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic