UKUTA wa Simba kwa msimu wa 2020/21 unashikilia rekodi ya kuwa namba kwa mabeki ambao wameruhusu nyavu zao kutikiswa mara chache.
Ni kazi ya Joash Onyango na Pascal Wawa ambao hawa walikuwa wakipewa majukumu ya kuwa viongozi katika eneo la kati kwa kumalizia mipango yote inayopangwa na wapinzani wao ya kuwafikia makipa wao Aishi Manula na Beno Kakolanya.
Katika mechi 34 ambazo Simba ilicheza walishuhudia jumla ya mabao 14 yakizama kwenye nyavu zao kwa msimu uliomeguka.
Pia wengine ambao walikuwa wakifanya kazi kwa ushirikiano eneo la beki ni Kened Juma ambaye naye ni beki wa kati pamoja na Ibrahim Ame hawa wote wawili ni wazawa.
Kwa upande wa pembeni kuna nembo mbili za taifa ambazo zilikuwa zikipambania kombe, kulia ni Shomar Kapombe na mshindani wake alikuwa ni David Kameta na kushoto nahodha msaidizi Mohamed Hussein mshindani wake alikuwa ni Gadiel Michael.
Kwa ukuta ambao uliruhusu mabao mengi ulikuwa ni ule wa Mwadui FC ambao uliruhusu jumla ya mabao 69 na ikiwa nafasi ya 18 ilikusanya pointi 19, msimu ujao itashiriki Ligi Daraja la Kwanza kwa sasa jina limebadilishwa inaitwa Championship.
0 COMMENTS:
Post a Comment