PITSO Mosimane, Kocha Mkuu wa Klabu ya Al Ahly mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa sasa msimu wa 2021/22 atakuwa na kijana wake anayekubali uwezo wake ambaye ni Luis Miquissone.
Ni Luis ambaye alikuwa anaitumikia Simba msimu wa 2020/21 na alikuwa miongoni mwa wale walioipa tabu timu hiyo yenye mkwanja wa kutosha Afrika.
Wakati ubao ukisoma Simba 1-0 Al Ahly ni Luis aliachia shuti kali kwa pasi ya mshikaji wake Clatous Chama na kuwanyanyua mashabiki wa Simba kwa shangwe kubwa jukwaani.
Mwingine ambaye naye amesepa na kuibuka ndani ya RS Berkane ya Morocco ni mtoa pasi ya mwisho kwa Luis anaitwa Clatous Chama wengi wanapenda kumuita Mwamba wa Lusaka.
Ilikuwa ni Februari 21 katika mchezo wa hatua ya makundi ambao ulikuwa na ushindani mkubwa huku Simba walikuwa wakipewa nafasi kiduchu ya kushinda mchezo huo.
Licha ya Simba kushinda mchezo huo waliweza kuwazidi mabingwa hao mara 10 wa Ligi ya Mabingwa Afrika katika suala zima la umiliki wa mpira pamoja na pasi za kutosha.
Rekodi zinaonyesha kuwa Simba walipiga jumla ya pasi 451 na Al Ahly walipiga pasi 425 na kwa upande wa umiliki wa mpira Simba ilikuwa ni asilimia 51 na Al Ahly ilikuwa ni asilimia 49.
Tunatarajia kwa uwezo wa Mungu wetu mambo msimu huu yatakuwa kuliko misimu yote iliopita
ReplyDeleteSimba ya Leo ni bora na ya muda mrefu kuliko Hiyo unayoizungumzia
ReplyDeleteCoast jana walikuwa bora sana kuliko mikia
ReplyDeleteKimyaaa
DeleteSimba haijashinda mechi hata moja tangu wachezaji wa maana wawili waondoke. Imetoka sare tatu hadi hivi sasa. Imetoka sare hadi na Coastal Union
ReplyDeleteSimba haijashinda hata mechi moja tangu wachezaji wake wa maana wawili waondoke. Imetoka sare mara tatu. Imetoka sare hadi na Coastal Union
ReplyDelete