September 27, 2021


MABINGWA wa taji ya Ngao ya Jamii leo wamesepa Bongo na kuwafuata wapinzani wao kwenye Ligi Kuu Bara, Kagera Sugar.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ilishinda taji la Ngao ya Jamii kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi.

Ilikuwa Septemba 25, Uwanja wa Mkapa ambapo bao la nyota mpya Fiston Mayele liliwamliza Simba mazima na kuwafanya waliyeyushe taji ambalo lilikuwa mikononi mwao.

 Mchezo huo wa kwanza wa Yanga unatarajiwa kuchezwa Septemba 29 siku ya Jumatano, Uwanja wa Kaitaba.

Msimu uliopita kwenye mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Kaitaba, Yanga ilishinda bao 1-0 na kusepa na pointi tatu mazima hivyo msimu huu wana kazi ya kulinda rekodi huku Kagera Sugar ikiwa na hesabu za kutibua rekodi.

Ushindi walioupata unawafanya wawafuate wapinzani wao kwa kujiamini katika kusaka pointi tatu muhimu.

3 COMMENTS:

  1. Bolingo ya Namanyele Hoyeeee! Sasebosaaaaa! Etutana etunana yango na yango! Asante Mopao kwa kufungua furaha Yanga Day

    ReplyDelete
  2. Mayele atakuwa mayala tusubiri hiyo J'5

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic