WAKATI Manchester United wakibanwa mbavu na Everton katika mchezo wa Ligi Kuu England kwa kuufanya ubao wa Old Trafford usome Manchester United 1-1 Everton kwa Chelsea ilikuwa ni kicheko kikubwa kwa kuwa ubao wa Uwanja wa Stamford Bridge ulisoma Chelsea 3-1 Southampton.
Yalikuwa mabao ya Trevoh Chalobah dakika ya 9, Timo Werner dakika ya 84 na Ben Chilwell dakika ya 89 huku lile la Southampton lilipachikwa na James Ward-Prowse dakika ya 61 na alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 77 baada ya kuonekana akimpa changamoto Jorginho anayenolewa na Kocha Mkuu, Thomas Tuchel.
Kadi hiyo inamfanya awe mchezaji wa nne ndani ya Southampton kuweza kufunga ndani ya mchezo na kuonyeshwa kadi nyekundu ambapo wengine waliowahi kufanya hivyo ni Peter Crouch ilikuwa Mei 2005, Sadio Mane ilikuwa ni Oktoba 2015 na Pierre Emile Hojbjerg ilikuwa ni Desemba 2018.
Kwa upande wa United wao bao lao lilipachikwa na Anthony Martial ilikuwa dakika ya 43 lilisawazishwa na Andros Townsend dakika ya 65 hivyo United ya Ole Gunnar Solskjaer inafikisha pointi 14 huku ikiwa sawa na Everton zote zimecheza mechi 7 ndani ya Ligi Kuu England.
0 COMMENTS:
Post a Comment