October 3, 2021


KATIKA wiki nyingine tena kampuni ya michezo na burudani Sportpesa imetoa bonus kwa washindi wake waliobashiri kwa usahihi mechi 12 kati ya 13 kwenye Jackpot yao ya kila wiki.

Mpaka hivi sasa Jackpot imefika shilingi 537,737,060 ambapo kila wiki huongezeka endapo mshindi hatopatikana.

Wiki iliyopita idadi ya washindi waliobet sahihi mechi 10 walikuwa 660 na kila mmoja aliondoka na Tsh 70,013, waliobet kwa usahihi mechi 11 walikuwa 83 kwa ujumla na kila mmoja akiondoka na kiasi cha shilingi 487,141 na wale waliobet kwa usahihi mechi 12 walishinda 15,610,066 kila mmoja.

Sportpesa huhakikisha washindi hawa wanakabidhiwa pesa zao mara tu mechi zote zikimalizika na endapo michezo isiyozidi mitatu ikiahirishwa basi droo ya wazi huchezeshwa ili kupata matokeo na ikiwa mechi zaidi ya tatu zimeahirishwa basi fedha zote hurudishwa kwenye akaunti ya mteja.

Waliojishindia 15,610,066 walikuwa nane kutoka sehemu mbalimbali nchini ambao ni Richard Magele kutoka Geita, kutoka Dar es Salaam ni Sengo Lubasha, Mohammedwaseem Gjartem na Ramadhan Chiwango, Enock Ernest kutoka Makoko, Musoma, Jabil Mwanjoa, Yusuph Jaivi kutoka Lindi na Amin Ally kutoka Kagera mjini.

Akizungumza mmoja wa washindi wa bonus Yusuph Jaivi kutoka Lindi alisema “Mimi ni mkulima wa Korosho ambaye kupitia bidhaa hii naweza kuongeza pato la taifa, nimeanza kucheza na Sportpesa tangu mwaka 2017 ambapo nadhani kampuni hii ilianzishwa.

“Nilitumia tsh 2000 kuweka bet ya Jackpot na kushinda moja kwa moja mechi 12 kati ya 13 na matarajio yangu kupitia hii pesa nitaweza kumuuguza mama yangu ambaye hivi sasa mwili umepooza, nitaendeleza biashara yangu kwa kununua mazao na nyingine kuweka kama akiba.

“Ndoto yangu kubwa ni kuja kushinda Jackpot maana nahakika itanibadilishia maisha yangu moja kwa moja, sijawahi kushinda bonus ila nimeshinda hizi bet za kawaida zaidi ya mara 5," amesema.

Akizungumza kutoka Sportpesa Sabrina Msuya, Meneja Uhusiano na Mawasiliano amesema: “Hivi sasa Jackpot yetu imefika 537,737,060 ambayo ni sawa na nusu bilioni hivyo basi ni wakati mzuri kwa wateja wetu wapya na wanaobet na Sportpesa kushiriki vilivyo kuwekeza kwenye kubet Jackpot.

“Kupitia Jackpot mteja anaweza kucheza double combination hadi mechi 7 ambayo inampa nafasi kuchagua matokeo mara mbili kwenye hizo mechi. Vile vile swala la bonus liko pale pale kuanzia mechi 10-12”.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic