NAHODHA wa Geita Gold, Jofrey Manyasi amebainisha kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Yanga.
Geita Gold inayonolewa na Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije mchezo wao wa kwanza ilipoteza pointi tatu baada ya kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Namungo FC ilikuwa Uwanja wa Ilulu.
Kesho inakibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Yanga ambayo imetoka kushinda bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Kaitaba.
Manyasi amesema:"Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Yanga na tunaamini kwamba tutapata ushindi na tumejiandaa.
"Wachezaji tunajua kwamba tumetoka kupoteza pointi mbele ya Namungo hivyo tuna kazi ya kufanya mashabiki wajitokeze kwa wingi,".
0 COMMENTS:
Post a Comment