October 1, 2021


 KAIMU Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, muda wowote anatarajiwa kutangazwa kuondoka kwenye nafasi hiyo, mara baada ya kukamilisha kipindi cha miezi miwili aliyokuwa akikaimu nafasi hiyo.

 

Uongozi wa Simba Julai 28, mwaka huu ulimtangaza rasmi Ezekiel Kamwaga kuwa kaimu ofisa habari mpya wa klabu hiyo kwa kipindi cha miezi miwili, kufuatia kuondoka kwa aliyekuwa msemaji wao, Haji Manara ambaye alijiunga na Yanga, muda ambao ulikamilika rasmi Septemba 28.

 

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kimelitonya Championi Jumatano, kuwa Kamwaga tayari amemaliza muda wake ndani ya Simba kama ilivyokuwa makubaliano yake na uongozi, na kwa sasa yupo kwenye mipango ya kuondoka nchini kwenda Uingereza kwa ajili ya masomo.

 

“Ezekiel Kamwaga tayari amekamilisha muda wake wa uongozi ndani ya Simba kwa kuwa alipewa miezi miwili pekee kutokana na kuwa na majukumu ya kwenda kwenye masomo nchini Uingereza, hivyo mpaka sasa yupo kwenye harakati za kuondoka,” kilisema chanzo hicho.

 

 Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu alisema: “Kama Uongozi bado hatujatoa taarifa rasmi juu ya nani atachukua nafasi ya Kamwaga, na hata wakati tunampa majukumu hayo tulisema atakaimu nafasi hiyo kwa miezi miwili, au zaidi hivyo kama kutakuwa na taarifa ya tofauti tutawajulisha.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic