October 3, 2021


 KIPA namba moja wa timu ya Simba ambaye amekusanya cleansheet (Cheza bila kufungwa) mbili ndani ligi amelipa mkopo aliokopeshwa na kipa namba moja wa Yanga, Diarra Djigui kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, wakati ubao ukisoma Simba 0-1 Yanga ni shuti la mguu wa kulia la Diarra lilipita kwenye miguu ya wachezaji watatu kisha likazama nyavuni ambapo lilianza kwa Diara, Farid Mussa huyu alitoa pasi kwa Fiston Mayele ambaye alimtungua Manula bao la ushindi.

Manula alipata somo na kusepa nalo kisha akalipa mkopo huo mbele ya Dodoma Jiji, Uwanja wa Jamhuri Dodoma ambapo Simba ilishinda bao 1-0 mbele ya Dodoma Jiji.

Alianza Manula kwa mpira mrefu akiwa nje ya 18 likakutana na Chris Mugalu ambaye alitoa pasi yake ya kwanza kwa msimu wa 2021/22 iliyokutana na Meddie Kagere aliyemaliza shughuli kwa kumtungua Hussein Masangala wa Dodoma Jiji.

Kwa maana hiyo ngoma imekuwa sawa kwa makipa hawa wawili ambao wanapewa nafasi ya kuweza kuonyeshana umwamba kutokana na kila mmoja kuwa na uwezo mkubwa katika kutimiza majukumu yake.

Pia jana wakati Yanga ikishinda bao 1-0 Diarra alikusanya clean sheet yake ya pili kwa kuwa mchezo wa kwanza hakufungwa mbele ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba.

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic