October 3, 2021


 UONGOZI wa Yanga umebainisha kwamba umesajili wachezaji chuma jambo ambalo linawafanya wawe na ukuta mgumu kama wa Berlin huku eneo la viungo ikiwa kazi ni kubwa.


Mkuu wa Kitengo cha Habari ndani ya Yanga, Hassan Bumbuli aliliambia Spoti Xtra kuwa dhamira kubwa ya kufanya usajili makini ni kuwa na chaguo la kufanya kwenye kila mechi ili wapate pointi tatu.


“Unaona kwamba kwenye mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar eneo la beki wa kati hakuanza Bakari Mwamnyeto ambaye ni nahodha lakini ilikuwa kama hakuna kilichotokea kazi ilifanyika na tukapata ushindi.Tuna ukuta kama ule wa Berlin.


“Kwa upande wa viungo hakuwepo Tonombe Mukoko kwa sababu ana ile adhabu aliyopewa kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii lakini bado eneo la kiungo lilisumbua  na kufanya vizuri.


Haji Manara, Ofisa Habari wa Yanga alibainisha kuwa uwezo wa ingizo jipya katika eneo la ulinzi Litombo Bangala ni moja ya wachezaji wenye uwezo mkubwa jambo linalomshangaza kila anapomtazama.


“Unakuwa na mchezaji mwenye uwezo mkubwa kama Bangala unadhani unahitaji nini kingine kama sio ushindi? Aina ya wachezaji wenye uwezo mkubwa kila mapigo kwake ni sahihi yupo yule Khalid Aucho huyu ni mzee wa pasi za uhakika kuna burudani kweli Yanga,” alisema Manara.


5 COMMENTS:

  1. Ukuta wa Berlin usingeruhusu magoli ya Rivers ya Nigeria.

    ReplyDelete
  2. Sofa za kijinga tu. Polisi yenye goli 4 unajifanya huoni ingakuwa Yanga au Sumba ungewasifia mafowadi wao. Yanga bado sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha umbumbumbu wewe! Ni kazi ya afisa habari wa Yanga kuzungumzia timu nyingine (Polisi)? Huko shuleni ulisomea ujinga?

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic