October 3, 2021


 KOCHA Msaidizi wa Simba Hitimana Thiery, raia wa Rwanda mambo bado hayajakuwa sawa kuhusu ishu ya vibali vya kazi.

Hitimana alitangazwa kuwa Kocha Msaidizi wa Simba bado hajakaa kwenye benchi la ufundi la timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Dider Gomes kutokana na kukosa vibali vya kazi.

Taarifa zimeeleza kuwa suala hilo kwa sasa linashughulikiwa na muda wowote itajulikana hatma yake ya kupata vibali vya kutendea kazi.

"Mwalimu Hitimana suala lake la vibali vya kazi bado halijapatiwa ufumbuzi kwa sababu viongozi walikuwa wanasubiri timu iweze kurudi Dar ilipokuwa Dodoma kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji na tayari timu imesharudi hivyo itafahamika hivi karibuni," ilieleza taarifa hiyo.

Kwa upande wa Hitimana kuhusu ishu hiyo alisema kuwa hawezi kuzungumzia jambo lolote kwa kuwa kuwa suala hilo linashughulikiwa na uongozi.


Chanzo:Spoti Xtra

12 COMMENTS:

  1. Hatutashangaa ukikuta na hiyu utopolo wameweka pingamizi kama la denis kibu ili kuipotezea muda simba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hakuna nchi yeyote ilyiyodai kuwa kibu ni raia wao bali kilichokuwa kinaendelea kwa kibu Yanga ilipigwa na Simba Kwenye mbio za kumuania, Yanga wakaamua kumsagia kunguni Kibu ili kuikomoa Simba. Kuna baadhi ya watumshi wa Serikali wanazi wa Yanga wanatumika kuihujumu Simba

      Delete
  2. Kibu Dennis alipokua akizichezea Mbao ya Mwanza pamoja na Mbeya City alikua raia wa Tanzania. Alipoibukia Simba sio raia wa Tanzania. Hivi hujuma hii kwa Simba hadi lini? Tunaomba uongozi wa Simba uamke maana sasa imetosha

    ReplyDelete
    Replies
    1. Una uhakika kila kitu kiki kwama unahusisha kuwa ni Yanga ? Kuhusu vibali Yanga ndio ofisi ya serikali inayotoa vibali?

      Delete
    2. Makoro bado hawataki kubadilika na kufuata taratibu zilizowekwa! Hii tabia ya 'short cut' itawatesa sana. Sijui ni ukoro umewazidi?

      Delete
    3. Kaa kimya kichwa kikubwa akili empty. Tutaendelea kuwanyoosha na vihujuma visivyo na msingi.

      Delete
  3. Aliyepeleka pingamizi tff kuhusu kibu ni nani, kuna nchi yoyote ilisema kibu ni raia wao? Mambo mengine ni kuabisha taifa letu, kumbuka kibu kachezea hadi taifa stars.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kufanya kosa kusihalalishe kosa!

      Delete
  4. Hivi tukiwa wakweli hao akina gsm na huyo injinia fake ni raia kweli kumzidi kibu?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kuna aliyewazuia? Na wewe kasome uwe injinia, ubongo lala!

      Delete
  5. Eti nasikia mo ni mhindi? Eti ni kweli?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic