October 3, 2021

 


OLE Gunnar Solskjaer, Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa hajutii kutomuanzisha kikosi cha kwanza nyota wake Cristiano Ronaldo katika mchezo uliokamilika kwa Manchester United kugawana pointi mojamoja na Everton. 

Baada ya dakika 90, ubao wa Uwanja wa Old Trafford ulisoma Manchester United 1-1 Everton na bao la United lilipachikwa  na Anthony Martial dakika ya 43 na lilisawazishwa na Andros Townsend dakika ya 65.

Kipindi cha kwanza Ole Gunnar alianza na Edinson Cavan na Anthony Martial katika Uwanja wa Old Trafford ikiwa ni mara ya kwanza kwa Ronaldo kuwekwa benchi ndani ya United tangu mwaka 2007 ilipokuwa hivyo kwenye mchezo wa Ligi Kuu England na katika mchezo huo United ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya West Ham United.

Solskjaer alipoulizwa kama anajutia kumuweka benchi Ronaldo alisema:"Hapana. Unajua ni lazima ufanye maamuzi mazuri na tuna msimu mrefu lazima uweze kuwaongoza wachezaji wako lazima ufanye uchaguzi sahihi.



"Anthony Martial amefanya kazi nzuri na amefunga bao pia Edinson (Cavan) alikuwa anahitaji dakika tu na alikuwa na uwezo wa kufunga. Lazima tufanya maamuzi kwa muda,".

2 COMMENTS:

  1. Huyo kocha Bora aondoke atuachie timu yetu analeta dharau et hajutii ☹️☹️

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic