LEO Oktoba 3 Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea ambapo kuna viwanja vitatu vitakuwa katika mikikimikiki ya kuhimili vishindo vya Wanaume 22.
Kwa upande wa Dar, Mtibwa Sugar watakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Tanzania Prisons kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Uhuru saa 8:00 mchana.
Itapigwa Dabi ya kibabe pia leo kati ya Mbeya City ya Mbeya pamoja na Mbeya Kwanza ya palepale Mbeya Uwanja wa Sokoine.
Pia Uwanja wa Ilulu itakuwa ni Namungo v Kagera Sugar.
0 COMMENTS:
Post a Comment