October 1, 2021


 KIUNGO kinda wa Azam FC, Khelffin Hamdoun, amefanikiwa kufuzu majaribio katika timu ya vijana ya Liverpool.


Hamdoun alienda mjini Liverpool, England mwezi uliopita ambapo alifanya majaribio na kufanikiwa kufaulu lakini ilishindikana kuingizwa kwenye usajili kutokana na dirisha kufungwa.


Kwa sasa bado yuko Liverpool na muda wowote kuanzia sasa anatarajia kurejea Bongo kujiunga na Azam.


Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Azam FC, Thabiti Zakaria, amesema kuwa: “Ni kweli Khelffin yupo Liverpool kwa ajili ya majaribio, ameweza kupita lakini shida imekuja usajili wa Liverpool umeshafungwa.


“Atarejea nyumbani mpaka usajili wa dirisha dogo utakapofunguliwa, Inshaallah ataenda tena.”

Kwa sasa Azam FC ipo Moshi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kesho, Oktoba 2, Uwanja wa Ushirika Moshi.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic